We at Hairpolitan Lifestyle Magazine are happy and proud to be official digital media partner of the Kipilipili Expo event 2017. In this article we chatted with the girls behind the awesome brand, Ziada and Basia, to find out more about the event. Read to find out why their focus is on natural hair, why they decided to put the Expo together, what their goals for the event are a what attendees can expect.

Sisi kama Hairpolitan Lifestyle Magazine tunafuraha na tunajivunia kushirikiana na Kipilipili na kuwa washiriki rasmi wa Kipilipili Expo 2017 kwa mwaka huu. Katika makala hii tulizungumza na Ziada na Basia ambao ni waanzilishi wa kampuni ya Kipilipili kuhusu shughuli hii ambayo inatarajia kufanyika Jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Soma zaidi kufahamu kwanini wameanzisha Expo hii, malengo ya shughuli hii na wahudhuliaji watarajie nini.

Photography by Elle Emmanuel

Who is Kipilipili? 

Kipilipili is an online retail store that caters for natural hair products. Our focus is lifestyle and making shopping for natural hair and beauty products a social experience. We cater for women, men and children. Our brand’s purpose is to inspire, empower and encourage women to embrace their natural beauty. We do this by emphasising on women being proud of their natural crowns and using them to exude confidence.

Kipilipili ni nani?

Kipilipili ni kampuni inayojihusisha na usambazaji wa bidhaa za nywele asilia kwa ajilii ya kina mama, baba na watoto. Tumejikita Zaidi katika kuwafunza na kuhamasisha hususani wakina mama kupenda na kuthamini uzuri wao wa asilia haswa nywele zao asilia.

Model: Basia Wellu • Photography by Elle Emmanuel

Is this the first Kipilipili Expo Event?

No, this will make it the second one. Our debut expo was in 2016, it was called Nywele Natural and Beauty Expo.

The purpose of these expos is to open up and give platform to local businesses in East Africa display their locally made products while we encourage customers especially who are natural enthusiasts to love and trust our own products. In addition to letting the Naturalistas mingle and get more information about natural hair and how to take care of it. This year we’ve also introduced a male category so they don’t feel left out!

Je, hii ni Kipilipili Expo ya kwanza?

Hapana, hii ni shughuli yetu ya pili kufanya. Shughuli ya kwanza kufanya ilikuwa inaitwa Nywele Natural & Beauty Expo ambako ilifanyika mwaka jana. Nia ya kufanya hizi expo, kwanza kabisa ni kuwahamasisha wateja kupenda na kuthamini bidhaa zinazotengenezwa hapa nyumbani tukimaanisha bidhaa za hapa Afrika Mashariki na kuamini kuwa bidhaa hizi kama za nje ya Afrika Mashariki pia zinafanya kazi.

La pili ni kuwaleta pamoja wapenzi wote wa nywele asili kuongea na kubadilishana mawazo na uzowefu wao kuhusu nywele asilia. Na la msingi Zaidi ni kutoa elimu juu ya urembo asilia kwa ujumla. Na kwa mwaka huu ili tusiwaache wakina baba nyuma, tumeongeza kipengele cha “Male Grooming.”

Models: Basia & Ziada • Photography by Elle Emmanuel

Why did you feel the need to host an Expo Event?

In this industry, there is still a lot of misconception about natural hair and products. People use products without the understanding of the product and how it works with their hair or skin, women get discouraged easily soon as they start the journey etc.

The purpose of the expos is for the audience to share their experiences and reminding them that they are not alone in this journey and to meet the producers and sellers of the products as well as experts in this field to get more information and by the time they are buying natural hair products they can make an informed decision.

Kwanini mmeanzisha hii Expo?

Katika sekta hii, kuna fikra nyingi kuhusu bidhaa za nywele asili na matumizi yake. Asilimia kubwa ya watumiaji wanatumia bidhaa bila kuwa na uelewa wa kutosha. Aidha anatumia bidhaa kwa sababu kasikia rafiki yake anatumia au kwa sababu kasoma sehemu kuwa bidhaa inafanya kazi, na pindi ambapo haifanyi Imani inatoweka, kumbe aidha hakutumia vizuri kama ipasavyo au bidhaa hiyo sio sahihi kwa nywele zake. Kipilipili Expo inawaleta watu pamoja, watengenezaji wa bidhaa, wauzaji wa bidhaa na pia wanunuaji, hapo watapata kuuliza maswali na kujuzwa kuhusu mambo mbalimbali ya nywele asilia.

Model: Ziada • Photography by Elle Emmanuel

What can attendees look forward to in terms of activities for the day?

FUN!! We will have panelists, influencers that are experts in their fields discussing and demonstrating about different topics, such as use of products, male grooming, basic natural hair and skin care, the basics of makeup and hands on protective styling.

People will also get to walk away with prizes for funky hair styles, funky styles (male category) and best dressed squad a.k.a squad goals. Of cause, it also goes without saying the audience will enjoy live music while they shop.

Tutarajie nini kwenye Kipilipili Expo kwa siku hiyo?

Watu watarajie kujifunza mengi kwani kutakuwa na majadiliano kuhusu mada mbalimbali ikiwemo matumizi sahihi ya bidhaa za nywele, male grooming, jinsi ya kutunza ngozi na nywele asilia, jinsi ya kutumia vipodozi, jinsi ya kutunza nywele usukapo n.k

Mbali na hapo zawadi zitatolewa kwa kundi litakalo vaa vizuri, mtu atakayekuwa mbunifu zaidi na mtindo wa nywele zake na pia mwanaume atakaye onyesha ubunifu zaidi kwenye mavazi yake. Bila kusahau watu watafurahia mziki mzuri huku wakiwa wanapita kwenye meza mbalimbali wakiwa wananunua bidhaa na kupewa elimu juu ya bidhaa hizo.

Models Basia & Ziada • Photography by Elle Emmanuel

What are your overall expectations & plans for the event?

A successful event to us means seeing attendees enjoy the experience and come out informed, educated and encouraged to embrace their natural beauty.

Nini matarajio ya Kipilipili expo 2017?

Kwetu sisi matarajio yetu ni kuona wahudhuriaji wanafurahia shughuli na wakitoka pale, wametoka na elimu zaidi juu ya nywele asilia na hata wakienunua bidhaa basi wanajua jinsi ya kutumia bidhaa hizo kwa usahihi na jinsi ya kutunza nywele zao bila kukata tamaa. Mbali na hapo pia kwa upande wa wauzaji kuhakikisha kuwa wanakutana na wateja wao na kuwaeleimisha juu ya bidhaa zao. Hapo tunakuwa tumeofungua mlango kati wa wauzaji na wateja.

Models: Basia & Ziada • Photography by Manifester Brand

When is the next event?

Kipilipili Expo is an annual event. However, we do have smaller and more intimate events every quarter where we bring in different experts to discuss about particular topics. These topics depend on the number of requests we get from both women and men. Visit our pages for more updates.

Kipilipili Expo inafanyika lini tena?

Kipilipili Expo hufanyika kila mwaka mara moja. Lakini kila baada ya miezi mitatu huwa tunafanya shughuli hususani kwa watu wa wachache hasa tukitazamia mada ambazo zina uzito zaidi. Kwa kufahamu Zaidi kuhusu shughuli zetu na huwa zinakuwa lini, tufuate kwenye mitandao ya jamii.

Models: Basia and Ziada • Photography by Elle Emmanuel

What’s new and happening in the natural hair space in Dar es Salaam, Tanzania that the world should know about?

Women in particular are truly embracing their natural hair. We have influencers and online communities that give this encouragement and more than ever women are so proud of taking ownership of their natural beauty and standing up to the mainstream. It’s because of this that we see a wave of entrepreneurs embarking in the production of products that cater for natural hair such as oils, butters etc.

Kuna kitu gani kipya kinaendelea kwenye uwanja wa nywele asilia kwa Dar es Salaam ambacho mngependa dunia kufahamu?

Kwa sasa nchini Tanzania sio Dar es Salaam peke yake, wanawake taratibu wanaanza kuelewa umuhimu wa kuwa na nywele zao asilia, kujikubalia, kujipenda na kujidhamini. Na kwasababu hii tunaona kumekuwa na ukuaji mkubwa wa wajasiriamali ambao wamejikita kwenye utengenezeji wa bidhaa kwa ajili ya nywele na asilia, vipodozi na nywele kwa ujumla. Hii inaleta hamasa sana katika soko la urembo.

Artwork created by Basia

Why did you approach Hairpolitan Lifestyle Magazine to be a partner?

Hairpolitan Lifestyle Magazine is the only magazine in East Africa that focuses on natural hair. As a partner Hairpolitan is in line with what Kipilipili represents.

Also giving this lifestyle magazine an opportunity to be in front of the Tanzanian natural hair community as we believe the magazine’s content caters for the whole East African audience.

Kwanini mmependa kushirikiana na Hairpolitan Lifestyle Magazine?

Hairpolitan Lifestyle Magazine ni gazeti pekee Afrika Mashariki ambalo limejikita zaidi katika kuongelea masuala ya nywele asilia. Kimawazo na matazamo wa shughuli zetu zimefanana wote tukiwa na lengo la kuhamasisha na kuendelea kusisitiza hususani wanawake kuthamini uzuri wao asilia, ni kwa sababu hii, tumeona kushirikiana na gazeti hili ili kuwa na uzito katika kufikisha ujumbe huu kwa walengwa.

Mbali na hapo, hili ni gazeti lenye tija sana na tungependa naturalistas hapa nchingi Tanzania kufahamu gazeti hili na kuwa wanalifuatila kupata elimu zaidi juu ya nywele asilia na kuona nchi jirani wanafanya nini katika Nyanja hii.

Photography Elle Emmanuel • Artwork by Basia

What are your contact details and where can people follow Kipilipili?
Kwa mawasiliano, mnapatikana wapi?

All our contact details are available in any of the above source.

Kwa mengi Zaidi, sisi hupatikana kupitia tovuti na mitandao ya jamii tajwa hapo juu.

To find out more about the event, click this link.
Kufahamu zaidi nini kilichojiri kwenye expo ya mwaka jana, bofya hapa.

You may also like...